Serikali imewaagiza makamanda wa Polisi na wakuu wa Magereza mikoa yote nchini kuhakikisha inawapa dhamana mahabusi wote wanaokidhi vigezo vya dhamana na kuharakisha upelelezi wa kesi kwa watuhumiwa waliopo katika magereza ili kujikinga na ugonjwa wa Covid -19.

Hayo yamesemwa na naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi, mhandisi Hamad Masauni wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika vituo mbalimbali vya polisi Jijini Dodoma.

Aidha Masauni amebaini kuwepo msongamano wa mahabusi katika vituo vya polisi huku akizungumza na baadhi yao ambao ilionekana kesi zao zinadhaminika na wengine wakaruhusiwa katika ziara hiyo.

“Maagizo ya Serikali na wataalamu wa afya ni kuepusha misongamano sasa nimetembelea kituo hiki cha kati nimekuta mahabusi wengine wamekaa siku kumi na nne na wengine wanaingia wakiwa wametoka nje, huko hali inayopelekea  msongamano mkubwa katika kituo hiki, na kuna mmoja nimekuta wamemuweka siku tatu hapa kosa lake wamemkamata tu anapita nje ya bunge hii sio sawa,” amesema Masauni

Hata hivyo amesema  natoa maagizo kwa Makamanda wa Polisi nchi nzima katika kukabiliana na ugonjwa wa corona wahakikishe mahabusi wote ambao kesi zao zinadhaminika watolewe, agizo hilon pia liende kwa wakuu wa magereza yote nchini kuhakikisha watuhumiwa wote kesi zao zinaharakishwa kupelekwa mahakamani.

“Wananchi wamekuja kuona ndugu zao waliopo mahabusu tunajua ni haki yao pamoja na kuwaletea chakula lakini muwahudumie haraka waondoke hii mikusanyiko imeshakatazwa ni hatari sana” amesisitiza Masauni.

Waitara akemea wanopuuza masharti ya kujikinga na Corona
Rwanda: Wanajeshi watuhumiwa kubaka raia, Amri ya Karantini