Baada ya aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Lawrence Masha kujivua uanachama wa chama hicho, baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA wametoa maoni yao na kujibu tuhuma alizozitoa zikiwa kama sababu za kujivua kwake.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii akisema safari ya kupigania usawa na haki ni safari ndefu, kwa yeye mwanaume kushindwa kuhimili safari hiyo ni aibu kwani kuna wananwake ambao bado wanaendelea kuhimili ugumu wa safari.

Naye Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari ameandika ujumbe wake akisema kuwa wanajua sababu za Masha kuondoka CHADEMA na sio zile ambazo amezitaja, na hata hivyo wanaheshimu mamuzi yake.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa chama hicho, Vicent Mashinji amesema kuwa Masha kuondoka CHADEMA ni haki yake kisheria, lakini ni vyema akaweka wazi ukweli wa sababu za yeye kuondoka.

Hata hivyo, Lawrence Masha hapo jana ametangaza kujivua uanachama wa CHADEMA akisema kuwa chama hicho hakina malengo ya kushika dola, kama ambavyo malengo ya vyama vya upinzani yanavyokuwaga.

 

Jeshi la Zimbabwe lakanusha kufanya mapinduzi
Milioni 10 zatengwa kwa atakayetoa taarifa za kigogo wa PCCB