Shirikisho la Soka Barani Africa ‘CAF’ limeiruhusu Klabu ya Jwaneng Galaxy ya Botswana kuingiza Mashabiki 1000 katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC.

Jwaneng Galaxy watakuwa wenyeji wa mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Taifa wa Botswana majira ya saa tisa alasiri kwa saa za Afrika Kusini sawa na saa Kumi kwa saa za Afrika Mashariki.

Hatua ya kuruhusiwa Mashabiki 1000 wa klabu hiyo, huenda ikawa faraja kwa Jwaneng Galaxy ambayo kesho Jumapili (Oktoba 17) itacheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Simba SC.

Wakati Galaxy wakipewa ruhusa ya kuingiaza Mashabiki 1000, Simba SC imepewa nafasi ya Mashabiki 15000 katika mchezo wa Mkondo wa Pili utakaochezwa Jumapili ijayo (Oktoba 24), Uwanja Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

TPLB, ZPLB zakutana Dar
Simba SC: Tupo tayari kuikabili Jwaneng Galaxy