Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limeruhusu Mashabiki 35,000 kuingia kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam, kushuhudia mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya mtoano, kati ya Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa siku ya Jumapili (Novemba 28) kuanzia majira ya saa kumi jioni.

‘CAF’ wametoa ruhusa ya Mashabiki hao kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya UVIKO 19.

Simba SC watakua wenyeji katika mchezo, huku ikitegemea uwepo wa Mashabiki hao kuwaongezea nguvu ili kufikia lengo la kushinda nyumbani kabla ya kwenda Uwanja wa ugenini nchini Zambia.

Kikosi cha Red Arrows kinatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam wakati wowote kuanzia leo Alhamis (Novemba 25), tayari kwa mchezo huo wa mkondo wa kwanza.

Red Arrows waitega Simba SC
Kilichonikuta baada ya kuolewa mke wa pili