Mashabiki wa klabu ya Arsenal ya England wameonyesha kuchukizwa na mwenendo wa kikosi chao katika michezo ya ligi kuu, na wameazimia kwa pamoja, kumtaka meneja Unai Emery atangaze kujiuzulu.

Mashabiki wa Arsenal wamemtaka meneja huyo kutoka nchini Hispania kuchukua maamuzi hayo, baada ya timu yao kulazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Watford.

Shinikizo la kumtaka Unai ajiuzulu, limekua likitokewa kupitia mitandao ya kijamii, kwa madai meneja huyo ameshindwa kuonyesha makali ya kuleta mabadiliko chanya.

Katika mchezo dhidi ya Watford, Arsenal ilionyesha kiwango dhaifu na kuwapa wapinzani wao kutoka nyuma na kusawazisha mabao yote mawili.

Nguli wa Arsenal, Paul Merson amekosoa mabadiliko ya Emery katika mchezo huo ambao Arsenal ilizidiwa kwa kiwango na Watford.

Timu ya Wartfod iliokua nyumbani ilipiga mashuti 31 kulinganisha na Arsenal iliyopiga saba huku kocha Sanchez Flores akiondoka uwanjani kwa tambo.

Mshambuliaji nyota Pierre-Emerick Aubameyang alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza kabla ya Tom Cleverley na mchezaji aliyetokea benchi Roberto Pereyra kusawazisha Watford.

Nikki Mbishi ampongeza harmonize kutoka WCB
Walimu wa masomo ya sayansi wanolewa Njombe