Katika pita pita za mtandaoni kuona yaliyojiri, nimekutana na haya maneno ambayo yanafikirika na yanaweza kuwa na ukweli ndani yake japo inawezekana kuwa bado ni mapema sana kusema hayo ila nimelileta kwenu wadau mlijadili.

Wakati Joh Makini ametoa wimbo akiwa amemshirikisha Davido, Kolabo hiyo ilisubiliwa kwa hamu, mategemeo na matarajio ya mashabiki yalikuwa makubwa walifanya kitu kizuri wimbo ulikuwa na mashairi mazuri ”kata leta”, lakini na thubutu kusema Sweet Mangi ilisumbua na kufanya vizuri zaidi kuliko hii ya kata Leta na Davido.

Kupitia mtazamo huo hasi mashabiki wa Joh wakaamua kusema ”Joh katoa wimbo na Davido kama hakijatokea kitu”

Msemo huo umegeuzwa kwa Diamond Platinumz mara baada ya kufanya mwimbo na Rick Ross maarufu kama Waka Waka mashabiki wanahoji.

Wanasema ”Diamond katoa wimbo na Rick Ross kama hakijatokea kitu”.

Inawezekana ikawa bado mapema kufikiria hivyo au kusema hivyo,  toa maoni yako juu ya mtazamo huo.

ZANU-PF yawafukuza wabunge 11
Marekani kuzikabili Urusi na China