Mshambuliaji wa majogoo wa jiji Liverpool, Daniel Sturridge amaeachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England, licha ya kuonyesha uwezo mkubwa wakati akicheza mchezo wake wa kwanza msimu huu wa 2015-16 mwishoni mwa juma lililopita.

Kocha Roy Hodgson, jana alitaja kikosi cha England ambacho kitaingia kambini mwishoni mwa juma hili, kwa ajili ya kujiwinda na michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya dhidi Estonia pamoja na Lithuania.

Hodgson aliwashangaza wengi, baada ya kutangaza kikosi chake pasina kumtaja mshambuliaji huyo ambaye alifanikiwa kuifungia Liverpool mabao mawili, miongoni mwa mabao matatu yaliyoipa ushindi klabu hiyo mbele ya Aston Villa.

Mashabiki wengi nchini humo waliamini kurejea vyema kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, huenda ingekua chachu kwa safu ya ushambuliaji ya timu ya taifa ya England katika michezo miwili itakayowakabili juma lijalo.

Katika hatua nyingine Hodgson, amemteua kiungo kinda wa klabu ya Tottenham, Dele Alli mwenye umri wa miaka 19 pamoja na mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Danny Ings mwenye umri wa miaka 23, kwenye kikosi chake ikiwa ni mara ya kwanza kwa wachezaji hao kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England.

Kikosi kamili kilichotajwa na Roy Hodgson tayari kwa mapambano ya michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016 dhidi ya Estonia pamoja na Lithuania, kwa upande wa makipa yupo Jack Butland (Stoke City), Joe Hart (Manchester City) na Tom Heaton (Burnley)

 Mabeki: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Kieran Gibbs (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Chris Smalling (Manchester United) na John Stones (Everton)

 Viungo: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Michael Carrick (Manchester United), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Jonjo Shelvey (Swansea City) na Raheem Sterling (Manchester City)

 Washambuliaji: Danny Ings (Liverpool), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Wayne Rooney (Manchester United), Jamie Vardy (Leicester City) na  Theo Walcott (Arsenal)

Gareth Bale Aitwa Kikosini Wales
Tanzia: Askari Wa JWTZ Wapotea Baharini, Wengine Wafariki Kwa Ajali Ya Basi