Tetesi za Usajili kutoka kwa Mabingwa wa Soka Tanzanai Bara Simba SC zinaeleza kuwa tayari kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama ‘ Tripple C’ ameshamalizana na Uongozi wa klabu hiyo, na kilichobaki ni kutambulishwa kwa Mashabiki  na Wanachama.

Chama anatajwa kuwa sehemu ya Usajili wa Simba SC kupitia Dirisha Dogo, akitokea RS Berkane ambako aliuzwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea kwa wakali hao wa Msimbazi.

Alipoulizwa kuhusu tetesi hizo Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC Ahmed Ally amesema, Mashabiki na wanachama wanapaswa kuwa watulivu, kwani Dirisha Dogo la Usajili halijafungwa, hivyo ni suala la muda tu, watajua nani na nani amesajiliwa klabuni hapo.

“Bado usajili unaendelea na usajili wa Tanzania ni tofauti na Ulaya ambao huwa wanaweka mambo wazi, tusubiri bado dirisha halijafungwa.”

Dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa Jumamosi (Januari 15), baada ya kufunguliwa Desemba 16, 2021, huku Simba SC ikiwa klabu pekee iliyokaa kimya hadi sasa kuhusu wachezaji waliowasajili.

Nabi asitisha mapumziko, awaita wachezaji kambini
Shiboub, Moukoro OUT Simba SC