Mashabiki wa Ali Kiba wameanzisha mashambulizi ya maneno dhidi ya kituo cha runinga cha MTV Base wakikitaka kuacha kumbania nyota wao huku wakicheza nyimbo za wasanii wengine wa Tanzania.

Hali hiyo imeibuka baada ya MTV Base kupitia Twitter kuanzisha mchuano wa kufahamu nani alikuwa msanii aliyefanya vizuri zaidi mwaka 2015, ambapo kati ya Diamond, Ommy Dimpoz, Ali Kiba na Diamond… King Kiba aliongoza.

Ali Kiba alipata asilimia 48, Diamond alipata asilimia 45, Vanessa Mdee alipata asilimia 7 na Ommy Dimpozi asilimia 0. 

Hali hiyo iliwafanya mashabiki hao kuanza kushusha makombora kwa kituo hicho ikikishinikiza kucheza video za Ali Kiba kwa madai kuwa wanazibania bila sababu za msingi.

Ali Kiba pia aliwahi kukilalimikiia kituo hicho akieleza kuwa kuna watu wanaomchezea mchezo usiofaa ili nyimbo zake zisichezwe.

 

Sababu za Wasanii Kukataa Kulipwa Kwa Nyimbo zao Kuchezwa Redioni/TV zawekwa wazi
Watumishi wengine Tisa watumbuliwa

Comments

comments