Baadhi ya mashabiki wa klabu ya Arsenal, wameonyesha kupingana na matarajio ya meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger ya kumkabidhi kitambaa cha unahodha beki kutoka nchini Ujerumani, Per Mertesacker.

Wenger anatarajia kufanya maamuzi ya kumtangaza nahodha mpya wa kikosi chake wakati wowote juma hili, baada ya kuondoka kwa Mikel Arteta aliyekua na jukumu hilo katika kikosi cha The Gunner msimu uliopita.

Arteta alitangaza kustaafu soka mwishoni mwa msimu uliopita, na tayari inaelezwa amejiunga na klabu ya Man City kama kocha msaidizi.

Kwa nyakati tofauti baadhi ya mashabiki wa Arsenal, wameonyesha hisia zao kupitia mtandao ya kijamii wa Twitter, kwa kushangazwa na tetesi za Mertesacker kuwa mbioni kukabidhiwa unahodha, kwa kudai mchezaji huyo hafai.

Baadhi yao wamekwenda mbali zaidi na kutoa ushauri kwa Arsene Wenger kwa kumtaka amfikirie beki kutoka nchini Ufaransa, Laurent Koscielny ama malinda mlango kutoka Jamuhuri ya Czech, Petr Cech katika nafasi hiyo.

Msimu uliopita kikosi cha Arsenal kiliongozwa na manahodha wasaidizi Koscielny na Mertesacker, kufuatia majeraha ya mara kwa mara yaliyokua yakimsumbua Mikel Arteta.

Baadhi ya ujumbe ulioandikwa na mashabiki wa Arsenal kuhusu suala la unahodha.

Demba Ba: Nitaendelea Kucheza Soka
Juventus FC Waigomea Man Utd