Hatimae uongozi wa klabu ya Aston Villa, umemalizana na meneja kutoka nchini Ufaransa, Remi Garde kwa kumfungulia mlango wa kutokea, baada ya kuchoshwa na huduma zake za ukufunzi tangu alipoajiriwa novemba 2 mwaka 2015.

Mwenyekiti mpya wa klabu ya Aston Villa, Steve Hollis pamoja na mkurugenzi David Bernstein walifikia maamuzi ya kumtimua kazi meneja huyo na kutoa taarifa wakati mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya England na Uholanzi ukiendelea usiku wa kuamkia hii leo.

Baadhi ya mameneja kama Nigel Pearson, Sean Dyche pamoja na Steve Bruce wanatajwa huenda mmoja wao akapewa jukumu la kuinusuru Aston Villa isishuke daraja msimu huu.

Katika utawala wa Garde, Aston Villa imefanikiwa kushinda michezo miwili kati ya ishirini iliyochezwa akiwa kama mkuu wa benchi la ufundi, hali ambayo imepelekea klabu hiyo ya Villa Park kuendelea kuburuza mkia wa msimamo wa ligi ya nchini England.

Pep Guardiola Aendelea Kuushinikiza Uongozi Wa Man City
Mayanja Ashikwa Na Kigugumizi Kuhusu Ubingwa