Mashabiki wa klabu ya Tottenham Hotspurs, wameonyesha kulipiza kisasi kwa kuvunja vyoo vya uwanja wa Emirates unaomilikiwa na mahasimu wao wakubwa wa jijini London Arsenal.

Hatua hiyo inadhamiwa kufanywa na mashabiki wa Spurs, kufutia kuchukizwa na kitendo kilichoonyeshwa na mashabiki wa Arsenal, wakati wa mchezo wa kombe la ligi (Capital One Cup) mwezi Septemba cha kung’oa baadhi ya mabango yayokua yametundikwa kwenye uwanja wa White Hart Lane.

Mashabiki wa Arsenal walifikia hatua ya kufanya hivyo kwa kudhaniwa huenda furaha ilikua imewajaa, kutokana na kikosi chao kuibuka na ushindi wa mabao matano katika mchezo huo wa mwezi Septemba, japo jeshi la polisi jijini London liliingia kati na kufanya uchunguzi wa kina na kubaini uharibifu uliokua umefanywa uwanjani hapo.

Kwa hatua hiyo mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Spurs, wamedhihirisha kulipa kisasi cha kuvunja makaro ya vyoo vya upande wa jukwaa walilokua wamekaa wakati wa mchezo wa jana, ambapo mambo yalimalizika kwa timu zote mbili kugawana point kufuatia sare ya bao moja kwa moja.

Hata hivyo uongozi wa klabu ya Arsenal, haujasema lolote kufuatia uharibufu huo, ziadi ya picha za tukio hilo kuanikwa hadhani katika mitandao ya kihabari pamoja na ile ya kijamii.

Arsenal pamoja na Spurs wamekua na uhasama wa kiushindani mkubwa katika soka, lakini katika miaka ya hivi karibuni, imeonekana mashabiki wa pande hizo mbili wamevuka mipaka na kuanza kuonyesha hali ya uvunjifu wa amani baina yao.

Klabu hizo mbili zote zina maskani huko kaskazini mwa jijini London, na zinapokutana kwenye michuano yoyote nchini England huwa kuna upinzani wa hali ya juu, japo wachezaji wanapomaliza mchezo huonyesha kupatana kwa kusalimiana na kukumbatiana tofauti na kwa baadhi ya mashabiki.

Rais Magufuli Afanya Ziara Ya Kushtukiza Muhimbili
Hatma ya Babu Seya na Mwanae Kuamriwa Mahakama ya Afrika