Umoja wa mashabiki wa timu ya soka ya ‘Kagera Sugar’ inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara wameiandalia timu hiyo futari iliyowajumuisha wachezaji wote wa timu hiyo,benchi la ufundi, viongozi wa timu pamoja na mashabiki ikiwa ni ishara ya kuonyesha umoja na upendo kwa timu yao.

Futari hiyo imeandaliwa mkoani humo wilayani Bukoba mkoa wa Kagera na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kiserikali na dini katika kuonyesha mshikamano baina ya mashabiki na timu.

Akizungumza katika futari hiyo mmoja wa viongozi wa umoja wa mashabiki ambaye ni katibu wa jumuiya hiyo, Alex Xavery ameutaka uongozi wa timu ya Kagera Sugar kuonyesha ushirikiano na mashabiki ili kuweza kuijenga timu.

“Timu yetu tunajua hali iliyonayo na sasa tunamuomba mungu tubakie kwenye ligi, tukuombe mwalimu uanze kuwa na malengo ya kuchukua ubingwa msimu ujao, zipo tetesi kuwa mashabiki tukiwa na nguvu tutaichukua timu irudi kwa wananchi, mimi niseme tu hilo sio lengo letu sababu hatuna uwezo wa kuiendesha timu, amesema Alex.

Kwa upande wake kocha mkuu wa timu hiyo, Mecky Maxime amewaomba radhi mashabiki hao kwa mwenendo mbaya wa timu kwasasa katika msimu huu, ambapo amesema kufungwa ni sehemu ya mchezo na kukili mbele ya mashabiki hao kuwa hali ya timu kwasasa sio nzuri.

Timu ya Kagera Sugar tayari ilicheza mehi yake ya 36 ya ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya timu ya soka ya Stand Utd kutoka Mkoani Shinyanga katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na kukubali kichapo kitakatifu cha goli 3- 1 kipigo ambacho kimeifanya timu hiyo kushuka kutoka nafasi ya 13 hadi nafasi ya 15 ya msimamo wa ligi hiyo ikiwa imecheza michezo 36 ikiwa na alama 43 huku vinara wa ligi hiyo wakiwa ni mabingwa watetezi wenye alama 85 baada ya kucheza michezo 34.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 18, 2019
CAF yatangaza gharama za tiketi nchini Misri