Mashabiki wa mwanamuziki wa hiphop nchini Marekani Lil Wayne wamemjia juu mara baada ya kutokuonesha ushirikiano wala kuguswa kufuatia kifo cha rapa mwenzake Nipsey Hussle ambae alipewa heshima ya mwisho siku ya jana kwenye ukumbi wa Staples Center mjini Los Angeles.

Mashibiki wa msanii huyo wamemshushia matusi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Hata hivyo ukimya wa Lily Wayne umehusishwa na sababu za kuzaa na Lauren London aliyekuwa mchumba wa Nipsey Hussle.

Mtoto wa Lil Wayne na London, Comeron Carter jana alipata nafasi ya kutoa neno la rambirambi kwa rappa Nipsey.

Hata  hivyo baada ya maneno ya kejeli na mazito ya mashabiki yamemgusa Lil Wayne na kuamua kuandika kwenye ukurasa wake wa twitter ‘’RIP NIP’’ asubuhi ya leo.

Aidha, ni siku 12 tu zimepita tangu mfalme huyo wa Los Angles kupigwa risasi kwenye duka lake la Marathon Clothes ambapo rapa Lil Wayne aliposti picha moja tu tangu aprili 8 na haikuhusiana na kifo hicho kitendo kilichosababisha mashabki wake kumjia  juu.

 

 

Video: Makonda akiomba chama cha walevi kuunga mkono Serengeti Boys
Video: Makonda ahaidi mamilioni Serengeti Boys wakifuzu michuano ya kombe la dunia