Uongozi wa Young Africans umesikitishwa na vitendo vinavyoshamiri kwa baadhi ya Mashabiki wa Klabu hiyo kuzomea na kutukana baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo na hata kupigana wenyewe kwa wenyewe.

Uongozi umewataka mashabiki kutambua wana umuhimu mkubwa kwa kuiunga mkono timu na wachezaji wao, pia umewasisitiza kupendana wao kwa wao na kukosoana kwa njia ya Amani.

Taarifa kwa Umma iliyotolewa na Kaimu Katibu mkuu Wakili Simon Patrick imeeleza kuwa, Uongozi wa Young Africans unatambua Changamoto ya mashabiki kuumia kwa sababu ya matokeo, lakini umesisiza ushirikiano wa mashabiki kwa wachezaji badala ya kuwachanganya kisaikolojia au kugombana wao kwa wao Jambo ambalo halina afya kwa ustawi wa Klabu hiyo kongwe hapa nchini.

Uongozi pia umewataka wana-Yanga wote nchini kuhakikisha wanawalinda wachezaji wao kwa mambo yote kama utamaduni wa Klabu hiyo ulivyo, huku ukiwahakikishia mashabiki utawalinda wachezaji wao wote kwa misingi ya amani na usawa, kama ilivyo dhima ya klabu hiyo inayosisitiza upendo na amani michezoni.

Aidha Klabu ya Young Africans imewaomba waandishi wa Habari za michezo hasa za Mitandaoni kuzigatia kanuni na maadili ya kazi zao kwani baadhi yao wamekuwa chanzo cha kuvuruga amani na utulivu wa timu yao  kwa kuwahoji mashabiki ambao wamekuwa wakitoa lugha zisizofaa kwa wachezaji na viongozi.

‘Mlitaka nife?’, Vanessa afunguka ‘mauzauza’ aliyokutana nayo kwenye muziki
Ajira: Makampuni 10 yatangaza nafasi za kazi, ziko hapa