Taarifa za Jeshi la Kongo, na ile ya Shirika la haki za Binadamu la Convention for the Respect of Human Rights zimesema, watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu, wameshambulia vijiji viwili mashariki mwa Kongo mwishoni na kuuwa takriban watu 20.

Mratibu wa Shirika hilo, Christophe Munyanderu amesema wapiganaji wanaodhaniwa kuwa wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF), waliwaua wakazi na kuharibu nyumba katika vijiji vya Kandoyi na Bandiboli katika jimbo la Ituri siku ya Ijumaa Agosti 5 na Jumamosi Agosti 6, 2022.

Msemaji wa jeshi la Kongo, Jules Ngongo amesema katika eneo la Ituri, takriban vifo 20 viliripotiwa na amethibitisha kuwa washambuliaji hao walikuwa wakitafutwa na vikosi vya wapiganaji wa Kongo.

Alice Kyanga, mmoja wa manusura wa kifo na ambaye Wazazi wake walikuwa miongoni mwa waliouawa nyumbani kwao siku ya Jumamosi amesema, “Ni vigumu sana kwangu kuwa kawaida baada ya nilipoona miili ya watu, ni ukatili sana koo zao zilikuwa zimekatwa, inaniuma inaumiza.”

Allied Democratic Forces (ADF), ni wanamgambo wa Uganda waliohamia mashariki mwa Kongo miaka ya 1990, na walihusika na vifo 1,050 vya ukatili mwaka 2021, kutoka vifo 599 kwa mwaka 2020, takwimu ambazo zimetolewa na data kutoka Kivu Security Tracker, inayofuatilia ramani ya ghasia katika eneo hilo.

Juni 2022, Wataalam wa Umoja wa Mataifa walisema hali ya usalama imezorota katika jimbo la Ituri na jirani la Kivu Kaskazini tangu Serikali iwaweke ADF chini ya utawala wa kijeshi mapema mwaka jana 2021.

Hata hivyo, Serikali ya Kongo ilitangaza hali ya kuzingirwa katika majimbo hayo mwezi Aprili 2021 ili kukabiliana na mashambulizi yanayoongezeka ya wanamgambo, ikiwa ni pamoja na mauaji ya mara kwa mara ya ADF inayohisiwa kuwa na uhusiano na kundi la Islamic State.

Uganda, pia imetuma wanajeshi wake wasiopungua 1,700 kusaidia jirani yake kupambana na ADF, baada ya kushutumu kundi hilo kuhusika na msururu wa mashambulizi ya mabomu mjini Kampala hapo mwaka jana 2021.

Wabunge waidhinisha Baraza jipya la Mawaziri
Watatu hawajulikani walipo, gari la Mbunge lachomwa moto