Baada ya kumtimua kocha Cedric Kaze na kikosi kukabidhiwa kwa Kocha mzawa Juma Mwambusi, kiosi cha Young Africans baadhi ya wachezaji wamerejea kambini kwa ajili ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu pamoja na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Wakati wachezaji wakirejea mazoezini, Uongozi wa Young Africans umeamua kuanza upya, huku ukiweka masharti mazito tofauti na iilivyokuwa wakati wa Kocha Cedrick Kaze.

Sharti mojawapo ni wachezaji wote lazima washinde kambini na hakuna kurudi uraiani mpaka msimu umalizike mwezi Juni, na ambaye hataki kufuata kanuni hiyo, atawajibishwa kwa mujibu wa taratibu za kinidhamu.

Habari zinaeleza kuwa Young Africans wameamua kufanya hivyo baada ya kubaini Kaze alikuwa akiwapa nafasi ya upendeleo ya kuondoka kambini hapo wachezaji kwa vipindi vifupi vifupi baada ya mechi, jambo wanalodhani lilichangia kuwatoa kwenye mstari tangu mzunguko wa pili uanze.

Kocha Cedric Kaze aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo baada ya kuongoza kwenye michezo 18 ya ligi akishinda 10, sare 7 na kupoteza mmoja amechimbishwa kikosi hapo Machi 7 kutokana na kile ambacho kimeelezwa kuwa mwendo mbovu wa timu hiyo.

Young Africans inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 50 baada ya kucheza jumla ya michezo 23.

Mrema: Mimi ni mzima wa afya
Msafara wa Makamu wa pili wa Rais Zanzibar wapata ajali