Mtu mmoja nchini Uganda anayejulikana kwa jina la Michael Aboneka amelishtaki kanisa la Watoto Church akipinga kanuni za utaratibu wa kufunga ndoa akieleza kuwa zinakwenda kinyume na katiba.

Aboneka amefungua kesi hiyo katika mahakama ya katiba iliyopo Jjini Kampala kulishtaki kanisa hilo ambapo baadhi ya waumini wameonyesha kuunga mkono taratibu hizo na wengine kupinga taratibu hizo.

Amesema kuwa Watoto Church, linawanyima vijana wengi haki yao ya kikatiba ya kufunga ndoa na wapenzi wao baada ya kutimiza umri wa miaka 18 kama katiba ya Uganda inavyosema.

“Kwanza wanasema nilazima upate barua kutoka kwa wazazi wa bibi harusi ambayo wanaita Baraka. Kwangu inakwenda na kinyume cha katiba kifungu 31 ya ndoa ya pili ni kukabidhi barua ya Dakitari ya majibu ya kupima virusi vya ukimwi kwa kanisa,”amesema Aboneka

Hata hivyo, Michael Aboneka ameongeza kuwa siyo kanisa la watoto pekee lenye utaratibu huo bali makanisa mengi nchini humo yanafanya hivyo na anasema ameiomba mahakama ya katiba kuanza mara moja kusimamisha kanuni hizo na anatarajia wiki hii mahakama inaweza kutoa jibu.

Bocco atamba kuiangamiza Majimaji FC
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Australia