Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika Bara la Afrika na ya 12 duniani kuwa mwenyeji Mashindano ya Dunia ya Urembo, Utanashati na Mitindo kwa Viziwi Duniani baada ya mashindano hayo kufanyika mara 12 baada ya kuanzishwa kwake.

Kauli hiyo imetolewa katika mkutano wa Waandishi wa Habari na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas na Rais wa Mashindano ya Urembo na Utanashati kwa Viziwi Duniani, Bonita Lee kutoka nchini Marekani.

Shindano hilo litafanyika leo JNICC Dar ea Salaam ambapo Rais Samia Suluhu Hassan atawakilishwa na Doroth Gwajima Waziri wa Jinsia, Wanawake na Makundi maalum na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa ambaye atakuwa mgeni maalum.

Dkt. Abbas amefafanua kuwa Serikali imewapa zawadi washindi wote wa shindano hilo la kidunia na viongozi kutembelea mbuga ya Wanyama ya Ngorongoro Oktoba 31,2022 baada ya kumalizika kwa shindano hilo ikiwa ni mwendelezo wa Royal Tour.

Amesema tukio hilo litarushwa na mitandao mbalimbali duniani ikiwa na pamoja na kituo cha televisheni cha AZAM ambacho kitarusha mbashara kupitia kipindi chake cha Sinema zet kuanzia majira ya saa mbili usiku.

Pia amesema katika tukio hili maalum itawajumuisha waalikwa zaidi ya 1000 ambapo filamu ya Royal Tour itaanza kuonyeshwa ili watu waone jinsi Tanzania ilivyobarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii.

Aidha, ameongeza kwamba burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa miziki mbalimbali zitaoneshwa kwa washiriki na ameomba washiriki kuwa tayari kupokea matokeo kutoka kwa majaji kwani hadi kufika hapa tayari wote ni washindi.

EMA yatoa tahadhari chanjo ya Uviko-19
Rais Samia kuzindua matokeo ya sensa jijini Dodoma