Mashindano ya watu wenye vipaji vya uigizaji yanayojulikana na kufuatiliwa zaidi nchini Tanzania ya Tanzania Movie Talent (TMT) yameingia mkataba na kampuni kongwe ya Teknolojia DataVision International ili kuwezesha washabiki wao kupiga kura kupitia simu za mkononi. Kampuni hio imewezesha upigaji kura huu kupitia Votex ambayo ni huduma inayopatikana kwenye mfumo wao wa huduma mbali mbali za simu za mikononi uitwao goMobile.

Votex inawawezesha washabiki na wafuatiliaji wa mashindano ya TMT kuwa na nafasi katika shindano hilo kwa kuchagua moja kwa moja mshiriki ambao wao wanadhani anastahili kuchukua zawadi ya shindano hilo. Mwakilishi wa kampuni ya DataVision International, bwana Benedict Ndunguru ameiambia Dar24 kuwa, “Kwa mda mrefu tumekuwa tukifanya kazi na mashindano mbali mbali kuwashirikisha washabiki wao kwa njia ya simu za mkononi. DataVision tumekuwa kwenye utafiti wa kuweze kuongeza huduma zetu za simu za mikononi ili kuwezesha wadau wetu kuwafikia na kuwashirikisha wadau/ wateja wao kirahisi zaidi na kwa uhakika”

Bendera Aipongeza Tff
Makamba: Anayemwaga Fedha Kusaka Urais Hafai