Kampuni ya usambazaji wa zana za kilimo Agricom Africa imezindua mashine ya kisasa ya ukaushaji wa nafaka za mpunga na mahindi nchini Tanzania.

Akizungumzia mashine hizo, Meneja wa kanda Nyanda za juu kusini, Joseph Manoni, amesema kwa sasa wakulima wataweza kukausha nafaka zao kwa muda mfupi na kuepukana na mlolongo na hasara kubwa ya upotevu na uharibifu wa mazao.

Kampuni hiyo imekuja na suluhu hiyo kwa wakulima katika kipindi hiki ambacho kilimo nchini Tanzania kimeshika kasi, ili kuwaondoa wakulima katika njia za asili za ukaushaji wa nafaka unaosababisha hasara, na upotevu wa viwango vya mazao hayo na hata kushindwa kuuzwa kimataifa.

Klopp azungumzia kinyonge EUROPA LEAGUE
Simba SC yaanza kusaka vifaa, Chama ndo hivyo tena!