Katibu Mkuu wa Chama  Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) Dkt. Vincent Mashinji amesema kuwa kuendelea kuhama kwa Madiwani na baadhi ya wanachama wa chama hicho chanzo chake ni rushwa na sio sababu nyingine kama wao wanavyotoa.
 
Ameyasema hayo mara baada ya kujiuzulu kwa madiwani wawili wa Chadema Mkoani Iringa na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
“Ukishakuwa kwenye nchi ambayo inaendekeza rushwa za kisiasa na kusumbua wala rushwa na mara zote mtu akishachukua mlungula ataongea kitu chochote anachokiona, maana hao waliojiuzulu jana wanasema hawaridhishwi na na CHADEMA kinavyojiongoza wao pia ni viongozi, sasa mimi nashangaa lakini hapo kikubwa ni rushwa ya kisiasa ndo imewafanya kuondoka,”amesema Mashinji
 
Aidha, Mashinji amesema kuwa sio tu madiwani ambao wanafuatwa na kupewa rushwa bali hata kuna wabunge na viongozi wa juu kabisa ambao wanafuatwa na kushawishiwa kwa kupewa rushwa.
 
  • Zitto: Tukio la Lissu lilinigharimu
  • Lissu: Bunge halijatoa hata senti moja
  • Polepole atishia kung’oa kigogo wa Chadema
 
Hata hivyo, mpaka sasa Manispaa ya Iringa Mjini imepoteza madiwani wa Kata sita ambao wote baada ya kujiuzulu walijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tanzia: Mke wa Kingunge Ngombale Mwiru afariki dunia
Upinzani wampinga Museveni