Serikali inatambua na kuthamini mchango wa hospitali za mashirika ya dini katika kutatua matatizo ya wananchi nchini.

Hayo yamesemwa na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu alipotembelea hospitali teule ya wilaya ya Rubya iliyopo wilayani Muleba

“Sera ya afya ni ileile hivyo tutaendelea kushirikiana katika kuboresha huduma zinazotolewa na madhebebu ya dini,hivyo bado ipo haja ya kufanya kazi nanyi”alisema

Waziri ummy alisema licha ya changamoto kubwa ya watumishi,wizara yake itaendelea kuwapangia watumishi katika hospitali hizo bila kudhoofisha utendaji wao

Alisema upungufu wa watumishi katika sekta ya afya nchini ni asilimia 48 ila kwa mkoa wa kagera upungufu ni asilimia 54,hivyo mkoa una uhaba mkubwa wa watumishi katika sekta ya afya.

Aidha,amesisitiza hospitali hizo kufuata taratibu za kiutumishi kwa kutoa taarifa sahihi Za kuajiri mbadala wa watumishi wastaafu na wale wanaokufa ili kuondoa watumishi hewa na wale wasiokuwa na sifa kwa kulipwa malipo yasiyo halali.

“Hatutamlipa mtumishi mshahara kwa keshi kwa watumishi wote waliopo kwenye hospitali teule zinazomilikiwa na mashirika ya dini bali tunahitaji watumishi wote walipe kupitia akaunti zao za bank ili kuondoa tatizo lililopo hivi sasa

Mkoa wa kagera ni miongoni mwa mikoa yenye hospitali nyingi zinazomilikiwa na mashirika ya dini nchini ambapo kati ya hospitali 14 za  mkoa huu,serikali ina miliki hospitali mbili tu
Sent from my Huawei Mobile

Waziri Mkuu Kuwa Mgeni Rasmi Kongamano la uwekezaji.
Madee Aonesha Kuguswa na Ujumbe wa Roma Kuhusu 'Tip Top' Kutekelezwa