Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa amebaini kuwepo kundi la watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (mashoga) 150 wanaosuka mpango wa kutaka kumuangusha baada ya kutangaza operesheni dhidi yao.

Makonda ambaye hivi karibuni aliapa kuwaondoa mashoga wote mkoani humo kwa kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, jana alieleza kuwaa Jeshi la Polisi lilinasa mpango huo ulisukwa kupitia kikao cha watu hao kilichofanyika katika baa moja iliyopo Kinondoni Mkoani humo.

Alisema tayari jeshi hilo limeshawatia nguvuni mashoga 8 kati yao ambao walihusika katika mpango huo.

“Nimebaini kuwa mashoga zaidi ya 150 waliketi katika baa moja Kinondoni wakipanga njama za kunimaliza kwa namna moja ama nyingine, lakini kutokana  na taarifa za kiintelijensia, watu kadhaa wengi wao wakiwa ni mashoga wameshakamatwa,” Makonda anakaririwa.

Hivi karibuni, Makonda alitangaza kufuta mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyodaiwa kujihusisha na kufadhili mashoga mkoani humo huku akiwataka watu wote wanaowafuatilia mashoga kwenye mitandao ya kijamii kuwaondoa mara moja kwenye akaunti zao (kuwa-unfollow).

Maafande Wa Ruvu Shooting Waachana Na Tom Olaba
Ratiba Ya VPL 2016-17 Yavuja, Young Africans Kuanza Na Kiporo