Uongozi wa klabu ya Real Sociedad ya nchini Hispania, huenda ukamfuta kazi David Moyes, ndani ya saa 24 zijazo kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi cha klabu hiyo kwenye ligi ya La Liga.

Moyes, ambaye alipewa ajira ya kukinoa kikosi cha klabu hiyo mwaka 2014, ameshindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo, kutokana na kushinda michezo miwili kati ya 11 ambayo imeshachezwa mpaka sasa huku Real Sociedad ikikamata nafasi ya 16 kwenye masimamo wa ligi ya nchini Hispania.

Uongozi wa klabu hiyo, unaamini ukifikia maamuzi ya kumfuta kazi meneja huyo kutoka nchini Scotland, huenda ikawa suluhisho la upatikanaji wa matokeo mazuri, kutokana na kuamini kwamba huenda mbinu zake zimeshindwa kuzaa matunda.

Maamuzi ya kufutwa kazi kwa Moyes, yanatarajiwa kuchukuliwa baada ya mkutano mzito wa maafisa wa klabu hiyo kukutana na rais Jokin Aperribay, ambaye amekua wa kwanza kuonyesha kuchoshwa na matokeo yanayoendelea kuwakabili.

David Moyes atakuwa na bahati mbaya kama lengo la kufutwa kazi litatimizwa, kutokana na mambo kumuendea kombo tangu alipoamua kuachana na klabu ya Everton mwaka 2013, na kwenda kujiunga na Man Utd kama mbadala wa Sir Alex Ferguson, ambapo alishindwa kufanya lililokua linakusidiwa Old Trafford na hatimae alisitishiwa mkataba wake.

Baada ya hapo alielekea nchini Hispania kujiunga na klabu ya Real Sociedad, na aliaminiwa huenda angekua na maisha ya mafanikio katika ufundishaji wa soka, lakini imeendelea kudhihirika bahati hiyo haipo kwake, na sasa anasubiri kurejea nyumbani.

Viti Maalum Vyapelekea Viongozi Wa Chadema Kujiuzulu
Chadema Watishia Kuhamasisha Mgomo Wa Wanafunzi Waliokosa Mikopo