Meneja wa klabu bingwa nchini Italia Juventus Massimiliano Allegri, amekanusha taarifa za kuwa mbioni kuondoka nchini humo, baada ya kuhusishwa na taarifa za kutaka kurithi kiti cha Mzee Arsene Wenger.

Allegeri amekanusha taarifa hizo zilizodumu kwa majuma kadhaa katika vyombo vya habari, dakika chache baada ya kikosi chake kukamilisha azma ya kutwaa ubingwa wa Italia kwa mara ya saba mfululizo, usiku wa kuamkia leo.

Juventus walikamilisha azma hiyo kwa kupata matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya AS Roma, ambayo yanaifanya klabu huyo ya mjini Turin kufikkisha alama 92 ambazo haziwezi kufikiwa na SS Lazio wanaoshika nafasi ya pili kwa kufikisha alama 88, huku mchezo mmoja ukisalia kabla ya msimu wa 20107/18 haujafikia kikomo juma lijalo.

Allegeri alikuwa napewa nafasi kubwa ya kuchukua majukumu kaskazini mwa jijini London kupitia vyombo vya habari, na alitajwa kuwa mtu sahihi ambaye huenda angefuata njia za Arsene Wenger, aliedumu na kikosi cha Arsenal kwa miaka 22.

“Kama hawatonifuta kazi, Nitaendelea kubaki hapa hapa kwa miaka mingine kadhaa,” Allegri anakaririwa.

Allegri mwenye umri wa miaka 50, alichukua jukumu la kuwa meneja wa Juventus miaka minne iliyopita baada ya kuondoka Antonio Conte, na mpaka sasa ameshaiwezesha klabu hiyo kutwaa mataji manne ya ligi.

Keita kutua Anfield kwa dau hili
Video: Diamond mbele ya mamaake amkana Hamisa Mobetto