Kiungo kutoka nchini Hispania, Juan Mata ameomba radhi kufuatia adhabu ya kadi nyekundu iliyomuangukia wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England, mwishoni mwa juma lililopita, ambapo Man Utd walikubali kibano cha kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya West Brom.

Mata, alionyeshwa kadi nyekundu iliyoambatana na kadi mbili za njano, baada ya kumchezea rafu kwa makusudi kiungo wa West Brom, Darren Barr Fletcher, alipokua katika harakati za kukokota mpira.

Mata, amesema haikuwa dhamira yake kufanya kosa hilo ambalo anaamini liliigharimu Man Utd katika mchezo huo, bali ilitokea kwa bahati mbaya, japo ilionekana kama alifanya kwa makududi kumchezea hovyo Fletcher.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, amewasilisha taarifa za kuomba radhi kwa mashabiki wa Man Utd katika moja ya Blog za nchini Hispania, ambapo amesisitiza kusamehewa na katu hatoweza kufanya kosa kama hilo tena.

Ameeleza kwamba hakuwahi kufanya kosa kubwa ambalo lilipelekea kuonyeshwa kadi nyekundu akiwa uwanjani, kwa zaidi ya michezo 500 aliyowahi kucheza, na kilichotokea siku ya jumapili anahisi ilikua ni kama tusi kubwa sana kwake.

Kwa mantiki hiyo sasa, Mata atakua nje ya uwanja wakati wa mchezo wa kombe la FA, utakaochezwa mwishoni mwa juma hili, kwa kutumikia adhabu hiyo inayomkabili ambapo Man utd watakua na kibarua cha kuwakabili West Ham Utd.

Ulimwengu Apewa Ruhusa Ya Kujiunga Na Stars
Massimiliano Allegri Avunja Ukimya