Mawaziri wa fedha wa kundi la mataifa yalioendelea zaidi kiviwanda G7 pamoja na wakuu wa benki kuu za nchi hizo wanatarajiwa kuwa na mazungumzo kuhusu virusi vya Corona.

Hali ya wasi wasi imeongezeka kwamba ugonjwa huo unaweza kudhoofisha hali ya uchumi wa dunia.

Wizara ya mambo ya fedha imethibitisha katika taarifa jana jioni kuwa waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin na mwenyekiti wa hazina ya taifa Jerome Powell wataongoza mazungumzo hayo ya G7 leo.

Waziri wa fedha wa Uingereza Rishi Sunak amerudia matamshi yake katika taarifa jana kuwa nchi hiyo iko tayari kwa kitisho hicho cha dunia.

Wakati taswira pana ya kiuchumi ikianza kuonekana, Uingereza iko tayari kutangaza msaada zaidi pale unapohitajika.

Mawaziri wa fedha wa mataifa ya Umoja wa Ulaya pia wanatarajiwa kufanya mazungumzo kwa njia ya simu kesho Jumatano.

Meya Iringa apewa siku 5 kujibu tuhuma nzito
Dkt. Shein afurahishwa taarifa ya BOT Zanzibar