Wamiliki wapya wa klabu ya Newcastle United wamesema wanataka kuibadili na kuwa timu kubwa kama Manchester City na Paris Saint-Germain, baada ya kukamilisha kuinunua kwa Pauni milioni 305.

Newcastle maarufu ‘Magpies’ sasa inakuwa klabu yenye wamiliki matajiri zaidi duniani.

Akizungumza na maelfu ya mashabiki waliokuwa wakishangilia makao makuu ya klabu hiyo St James’ Park, Staveley alisema:”Tunataka kuona mataji.

“Lakini mataji yanahitaji uwekezaji, muda, subira na ushirikiano.”
Wamiliki hao wamependekeza Kocha wa sasa wa Leicester City, Brendan Rodgers kuwa mwalimu mpya wa Newcastle.”

FIFA yaombwa kuiadhibu Real Madrid
Pogba aitia wazimu Manchester United