Zabuni zilizorekebishwa za kuinunua Klabu ya Manchester United bado hazijafikia kiwango kinachotakiwa na familia ya Glazer, ingawa bado kuna matumaini ya kuiuza, kwa mujibu wa ESPN.

Ofa za pili ziliwasilishwa na wahusika juma lililopita, wakiwamo Sheikh Jassim Bin Hamad Al Thani, Sir Jim Ratcliffe na Thomas Zilliacus.

Vyanzo vimeiambia ESPN kwamba zabuni kutoka kwa Sheikh Jassim na Ratcliffe zimeongezwa kutoka takriban Pauni Bilioni 4.5, lakini zimesalia chini ya bei inayotakiwa ya karibu pauni bilioni sita – ingawa kuna matumaini kwamba Glazers bado wanaweza kukubali bei ya maelewano kuruhusu kuiuza klabu hiyo ya Old Trafford.

Baada ya ofa ya hivi karibuni, wazabuni wanasubiri kusikia kutoka kwa Raine Group, Benki ya Marekani inayofanya kazi na Glazers katika mchakato wa kuiuza klabu hiyo.

Wafanyakazi wa United wameambiwa kutarajia “uwazi” juu ya hali ya umiliki ifikapo mwishoni mwa msimu.

Vyanzo vimeiambia ESPN kwamba bado ni “biashara kama kawaida,” ingawa kuna kukubalika kwamba upanuzi wa mikataba kwa wachezaji muhimu ikiwa ni pamoja na Marcus Rashford-na dirisha la uhamisho wa majira ya joto.

Wakati huo huo, wamiliki wapya wanaweza kutaka kufanya mabadiliko makubwa kwenye muundo wa klabu, ambayo inaweza kuhatarisha awamu inayofuata ya ujenzi wa kikosi chini ya kocha Erik ten Hag.

Baadhi ya vyanzo vimetaja usumbufu uliosababishwa na Todd Boehly baada ya kuinunua Chelsea, ambayo ni pamoja na kumtimua kocha Thomas Tuchel na nafasi yake kuchukuliwa na Graham Potter miezi minne tu baada ya ununuzi wake kukamilika.

Ten Hag amefanya kazi vizuri na mkurugenzi wa soka, John Murtough na timu yake tangu alipoteuliwa kuwa kocha msimu wa majira ya joto uliopita, huku Mholanzi huyo akiwa tayari ameshinda Kombe la Carabao katika msimu wake wa kwanza.

Singida Big Stars wanautaka ubingwa
Chamberlain ajiweka njia panda England