Watu wasiojulikana wamevamia matawi mawili na mabaraza matatu ya Chama Cha Wananchi (CUF) mkoa wa Kusini Unguja na kuchana bendera zilizokuwa kwenye milingoti.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea jana usiku wa manani katika Shehia ya Uzi mkoani humo na kuzua taharuki, ikiwa ni siku moja tangu Mahakama Kuu ibatilishe uteuzi wa wajumbe wa baraza la wadhamini wa chama hicho wa kambi ya mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na wale wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

Kutokana na uamuzi huo, waliokuwa wajumbe wa Baraza la Udhamini kabla ya mgogoro kati ya kambi hizo mbili wanaendelea kuhudumu.

Mkurugenzi wa Siasa na Habari wa CUF katika jimbo la Tunguu, Juma Ali ameliambia gazeti la Mwananchi kuwa bado hawajafahamu watu walifanya tukio hilo lakini wameripoti kwenye vyombo vya usalama.

“Kwa vile chama chetu kinaheshimu sheria, hatutafanya lolote lile lililo kinyume na sheria, badala yake tutafikisha suala hili kunakohusika.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Salim Abdallah Bimani alieleza kushangazwa na tukio hilo ambalo amelielezea kuwa sio la kiungwana.

Meneja afia kwenye kiti akizungumza na waandishi wa habari
Video: Meneja afariki dunia akihutubia wanahabari, Kifungo miaka 45 kwa mauaji tembo 430