Shirika la Umeme TANESCO, linapita kipindi kigumu cha upungufu wa umeme unao sababishwa na ukame na matengenezo ya mitambo ambapo jumla ya Megawati 300 – 350MW zimepungua katika uzalishaji kwa siku za hivi karibuni.

Vituo vilivyoaathiriwa na ukame ni pamoja na Kihansi (17MW vs 180MW, 63 hauzalishwi), Pangani (10MW vs 68MW, 58 hauzalishwi), Mtera (175MW vs 180MW, 5 hauzalishwi), Nyumba ya Mungu (3MW vs 8MW, 5 hauzalishwi).

Aidha, vituo vilivyo kwenye Matengenezo ni Kidatu (150MW vs 200MW, 50 hauzalishwi), Ubungo III (32MW vs 112MW, 80 hauzalishwi), Kinyerezi II(195MW vs 248MW, 53 hauzalishwi), ambapo jumla ya umeme ambao hauzalishwi kwa sababu ya ukame na matengenezo ni Megawati 414 hadi kufikia Novemba 23, 2022 asubuhi.

Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande (kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu hatua zinazoendelea kuchukuliwa kukabiliana na mgao wa umeme.

Hata hivyo TANESCO inasema hatua za muda mfupi zilizochukuliwa ni pamoja na kuharakisha matengenezo ya mitambo hiyo, ambapo inatarajiwa Megawati 90 zitapatikana kupitia mpangilio wa Mashine moja ya 40MW ya Ubungo III , kurudi tarehe 25.11.2022.

Hatua nyingine ni Mashine ya Kidatu 50MW kurudi 28.11.2022, Mashine mbili za Ubungo III 40MW kurudi kabla ya mwisho wa Disemba, na Kupatikana mashine mpya ya Kinyerezi I 90MW kabla ya mwisho wa Desemba.

Aidha, ukarabati ukikamilika kama ulivyopangwa itasaidia kupata Megawati 220 kwenye uzalishaji na kupunguza kadhia hii ya umeme huku mipango ya muda ambayo itapatikana mwezi Februari ni mashine nyingine ya Megawati 90 kuanza kuzalisha umeme na kufikisha jumla ya Megawati 310.

Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande (kulia), akizungumza na waandishi wa habari hii leo Novemba 23, 2022.

Hata hivyo, TANESCO imesema kwa kipindi hiki mvua zikipatikana hali ya umeme itaimarika mapema zaidi endapo hakutakuwa na hitilafu nyingine itakayo jitokeza na itatoa taarifa kila wiki kwa njia ya kukutana na waandishi wa habari na kila siku kupitia tovuti ya club house.

16 wapoteza maisha maporomoko mgodini
Urusi kupewa hadhi mdhamini wa ugaidi