Klabu ya Olympique Marseille ya nchini Ufaransa imelenga kumsajili beki wa kulia wa Arsenal Mathieu Debuchy, wakati wa dirisha dogo la usajili.

Gazeti la The Sun limeripoti kuwa, beki huyo ana nafasi kubwa ya kuondoka klabuni hapo kutokana na changamoto za kutokucheza katika kikosi cha kwanza kumkabili tangu aliporejea mwanzoni mwa msimu huu akitokea Bordeaux alipokua amesajiliwa kwa mkopo.

Meneja wa Olympique Marseille Rudi Garcia, anatajwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha beki huyo mwenye umri wa miaka 31.

Garcia anaamini Debuchy bado ana uwezo mkubwa wa kucheza soka, na kama atafanikiwa kumsajili mwezi Januari wakati wa dirisha dogo la usajili kutafanikisha kuongeza chachu ya ushindani ndani ya kikosi chake.

Mwishoni mwa juma lililopita Debuchy alianzishwa katika kikosi cha kwanza cha Arsenal kilichokabiliana na AFC Bournemouth, lakini ilimchukua dakika 15 kabla ya kutolewa nje ya uwanja kufuatia jeraha la misuli ya paja.

Debuchy alisajiliwa na Arsenal mwaka 2014 akitokea Newcastle Utd.

Mbadala Wa Dani Alves Aanza Kusakwa
Virgil van Dijk Kuzipotezea Liverpool, Everton?