Waziri wa Elimu nchini Kenya Fred Matiang’i amesema moto uliozuka katika bweni la Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Moi jijini Nairobi, na kusababisha vifo vya wanafunzi tisa na wengine kujeruhiwa ulianzishwa kwa makusudi.

Matiang’i ameeleza kuwa uchunguzi wa awali umeonesha wazi kuwa, mkasa huo haukuwa ajali na tayari polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.

Aidha, Waziri huyo ambaye pia anakaimu kama Waziri wa Usalama, ameeleza kuwa Polisi wamemfahamisha kuwa wamepata taarifa za uhakika kuonesha kuwa moto huo ulianzishwa makusudi.

Shule hiyo imefungwa kwa wiki mbili, wakati huu wanafunzi, wazazi na walimu wakiendelea kuomboleza.

Katika tukio hilo la moto Jumamosi wanafunzi 51 walijeruhiwa na wamepelekwa Hospitali ya Nairobi Women akiwa na majeraha ya viwango mbalimbali.

Jumla ya wanafunzi 40 walitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani wakati wengine 11 walilazwa hospitali na kati yao watatu walikuwa na majiraha mabaya sana.

Mpaka sasa Idadi ya vifo katika ajali hiyo imeongezeka kufikia tisa, ambapo msichana mmoja mwengine ambaye alilazwa hospitali ya Nairobi Women alifariki dunia kutokana na majeraha ya moto.

Mwaka uliopata, mabweni ya shule za sekondari 100 yaliteketezwa moto katika visa ambavyo pia viliripotiwa kuwa vya makusudi.

Ufisadi waponza mkataba Mlimani City
Mtoto wa Lil Wayne awatoa hofu mashabiki