Hatimaye Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza matokeo ya uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya Urais visiwani Zanzibar akimtaja Dk. Ali Mohammed Shein kuwa mshindi wa nafasi hiyo.

Dk. Ali Mohammed Shein akikabidhiwa cheti cha ushindi na Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha

Dk. Ali Mohammed Shein akikabidhiwa cheti cha ushindi na Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha

Kwa mujibu wa Jecha, Shein amepata ushindi wa kishindo wa kura 299,982 ambazo ni sawa na asilimia 91.4. Nafasi ya pili imeshikiliwa na mgombea urais wa ADC, Hamad Rashid aliyepata kura 9,734 sawa na asilimia 3, huku Maalim Seif Sharif Hamad (CUF) akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 6,076 sawa na asilimia 1.9.

Kutokana na matokeo hayo, Dk. Ali Mohammed Shein ndiye atakayeendelea kuiongoza Zanzibar kwa muhula wake wa mwisho kwa mujibu wa Katiba.

Hatma Ya Patrick Liewig Ipo Mikononi Mwa Viongozi Wa Stand Utd
Manny Pacquiao apigwa marufuku hii Marekani