Baada ya kuibuka kwa Vurugu katika ukumbi wa Bomas ambao unatumika kutoa matokeoa ya Urais nchini Kenya, na Polisi kuingilia kati kuamulia ugomvi ikiwa ni dakika chache baada ya Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, Wafula Chabukati kuingia ukumbini, hatimaye hali imekuwa shwari na utaratibu wa kawaida wa utoaji wa matokeo unaendelea.

Baadhi ya watu, walianza kurushiana ngumi na kutupiana viti kwa sababu ambazo bado hazijafahamika huku ikidaiwa kuwa Mgombea wa Urais wa Azimio Raila Odinga amegoma kuingia ndani ya ukumbi huo, hadi pale mawakala wake watakapopatiwa matokeo na kujiridhisha, na kwamba imearifiwa kwamba kuna mambo ambayo bado hawajakubaliana na hivyo haitawezekana kutoa matokeo.

Awali, matokeo hayo walikuwa yatangazwe muda wa saa tisa alasiri, lakini yaliahirishwa hadi muda wa saa kumi jioni, ambapo mpaka tunachapisha Habari hii kulikuwa bado, hakuna muafaka wa matokeo hayo na tayari matangazo ya luninga ya moja kwa moja yalikatwa kwa muda huku sababu nyingine zikitolewa kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo IEBC ilikuwa haijayaweka sawa na ulinzi umeimarishwa.

Kenya, ilifanya uchaguzi wake wa kitaifa Agosti 9, 2022 ambapo mpaka matokeo yanatarajia kutangazwa hii leo Agosti 15, 2022 wagombea wawili yaani Raila Odinga na William Ruto walikuwa wanachuana vikali na kura zao zilikuwa hazijapishana kwa kiwango kikubwa.

Ruzuku yawakutanisha pamoja Wadau wa AZAKI
Matokeo Kenya: Ngumi zarushwa ukumbi wa matangazo, Tume yagawanyika.