Hatimaye jimbo la Arusha Mjini limepata mbunge atakayeliwakilisha kwa kipindi cha miaka mitano huku kukiwa hakuna mabadiliko katika kiti hicho kilichokuwa kinakaliwa na mbunge wa Chadema, Godbless Lema.

Kwa mujibu wa matokeo rasmi ya uchaguzi huo mdogo uliofanyika jana, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Juma Iddy amemtangaza Godbless Lema kuwa mshindi baada ya kupata kura 67,250,353 sawa na asilimia 65.9 huku mshindani wake mkuu, Philemon Mollel wa CCM akipata asilimia 34.4.

Msimamizi huyo alitangaza kuwa watu waliojiandikisha ni 317.814, waliojtokeza kupiga kura ni 105,800 sawa na asilimia 32.83 na kwamba kura halali ni ni 104,353. Zaidi ya nusu ya idadi ya waliojiandikisha hawakujitokeza kupiga kura.

Wagombea wengine waliowania nafasi hiyo waliachwa kwa mbali, ambapo mgombea wa ACT-Wazalendo alipata kura 342 sawa na asilimia 0.3. Zuberi Mwinyi wa CUF aliyepata kura 106 ambazo ni sawa na asilimia 0.1 huku Makama Rashidi wa NRA aliyepata kura 43 sawa na asilimia 0.04.

Kilichojili Baada Ya Madiwani Wa CCM Geita Kushindwa Kusoma Kiapo Kwa Kukosa Elimu
Safari za Madiwani Zafutwa, Watakiwa Kutembelea Vijiji