Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC Seleman Matola amafichua siri ya ubora wa wachezaji Pappe Osusman Sakho na Peter Banda, ambao wameonyesha kiwango bora cha soka kwa siku za karibuni.

Matola ameweka wazi siri hiyo baada ya wachezaji hao wawili kuisaidia Simba SC kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Sakho aliifungia Simba SC bao la kuongoza katika mchezo huo, huku Banda akisababisha bao la pili kwa timu hiyo, kufuatia mpira alioupiga langoni mwa Mtibwa Sugar kumshinda Mlanda Lango Sahaban Kado aliyejifunga mwenyewe.

Matola amesema baada ya kukabidhiwa jukumu la kukaimu nafasi ya Kocha Mkuu kwenye kikosi cha Simba SC, alizungumza na wachezaji hao ili kufahamu changamoto wanazopita, hadi kushindwa kuonyesha uwezo wao halisi wanapopewa nafasi.

Amesema baada ya kufanya hivyo walimthibitishia wapo tayari kupambana, lakini endapo watapewa uhuru wa kucheza katika maeneo huru, ili kuisaidia timu.

“Nilikaa nao hawa wachezaji, wakaniambia hawapendi kupangiwa nafasi maalum uwanjani, wanataka uhuru wa kucheza kwa kujiachia, nilijaribu kufanya hivyo, wamenithibitishia kwa vitendo, leo wanaisaidia timu kushinda.”

“Mara kadhaa wanapocheza pamoja wanakubaliana wao wenyewe kubadilishana nafasi, nadhani hilo linaonekana uwanjani na kila mmoja ameshuhudia, wana elewana sana, mimi kama kocha ninafurahishwa na mwenendo wao.” Amesema Matola

Sakho aliifungia Simba SC katika dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa ushindi wa 3-0, kisha akafanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya KMC FC iliyokubali kichapo cha 3-0, jana Alhamis aliifunga Mtibwa Sugar iliyokubali kisago cha 2-0.

Harrison Mwendwa atua Dar es salaam
Msomera kumenoga, wahamiaji wasifia juhudi