Beki wa kati wa Bayern Munich Mats Hummels amemuomba meneja wa Man Utd Jose Mourinho, kumpa nafasi zaidi kiungo Henrikh Mkhitaryan kwenye kikosi cha kwanza cha Mashetani hao Wekundu.

Hummels aliliambia gazeti la Daily Mail kuwa  “ukimpa nafasi ya kucheza utaona ni kwa jinsi gani Mkhitaryan alivyo bora nina uhakika asiIimia 100 ni mmoja wa viungo bora niliowahi kucheza nao, niliona sehemu ya mchezo wao dhidi ya Feyenoord na niliona uzuri alionao akiwa dimbani, alicheza hivyo msimu uliopita akiwa Dortmund”.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 ameanza mechi ya pili katika ligi kuu nchini Uingereza baada ya kumfurahsiha  Mourinho katika mechi za ligi Europa dhidi ya Feyenoord na kombe la ligi dhidi ya West Ham United.

Pep Guardiola: Man Utd Huenda Wakamaliza Nafasi Ya Nne
Polisi Kagera yataja sababu ya kifo cha mchezaji wa Mbao FC uwanjani