Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Ligi ya Wanawake ‘Simba Queens’ Matty Mseti amekanusha uvumi wa kutimia Yanga Princess, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Edna Lema ‘Mourinho’.

Edna alijizulu nafasi yake ya Kocha Mkuu Young Princess juma lililopita, baada ya kuuandikia barua Uongozi wa Young Africans, na kupata baraka zote kutoka kwa mabosi wake.

Matty amekanusha taarifa hizo baada ya uvumi wa kuikacha Simba Queens kuendelea kusambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, ambapo amesema bado yupo yupo sana Msimbazi.

Matty ameandika: “Sina sababu ya kuondoka Simba Queens C.E.O wangu Barbara Gonzalenz ni mfano bora kwa caree na maisha yangu.”

“Naona kazi yake kwa macho yangu ni mtu muelewa sana na uwezo wake wa kufikiria siyo wa kawaida,  Najivunia kuwa na boss Barbara.”

Matty, amekua msaada mkubwa kwa bosi wake Mussa Hassan ‘Mgosi’, na kupelekea Simba Queens kutwaa ubingwa wa Ligi Ku ya Wanawake mara mbili mfululizo.

Neymar: Afrika hawajitumi
Young Africans yasambaza upendo Tabora