Mechi namba 1 Kundi B (Pepsi 1 v Madini 1). Pepsi imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kwa kuchelewa kwenye kikao cha maandalizi (pre match meeting), na pia kufika uwanjani. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.

Mechi namba 9 Kundi B (Madini 1 v Kilimanjaro Heroes 1). Kilimanjaro Heroes imepewa Onyo Kali kwa kuchelewa kikao cha maandalizi (pre match meeting) kwa dakika 16. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.

Mechi namba 11 Kundi B (Kilimanjaro Heroes 1 v African Sports 1). African Sports imepewa Onyo Kali kwa kuchelewa kufika uwanjani, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(9) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo. Kanuni hiyo inatika timu kufika uwanjani dakika 60 kabla ya mechi kuanza.

Mechi namba 4 Kundi C (Green Warriors 1 v Mkamba Rangers 0). Klabu ya Mkamba Rangers imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kutohudhuria kikao cha maandalizi ya mechi, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.

Mechi namba 5 Kundi D (Milambo 1 v Area C 0). Milambo imepewa Onyo Kali kwa kuwakilishwa na maofisa pungufu kwenye kikao cha maandalizi ya mechi. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.

Mechi namba 12 Kundi D (Milambo 0 v Mashujaa 1). Milambo imepewa Onyo Kali kwa kuwakilishwa na maofisa pungufu kwenye kikao cha maandalizi ya mechi. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.

Pia Mwamuzi wa Akiba, Rajab Said amepewa Onyo Kali kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi kwa dakika 6. Adhabu ya Mwamuzi ni kwa mujibu wa Kanuni ya 83(5) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Mechi namba 15 Kundi D (Area C 1 v Mashujaa 0). Mashujaa imepewa Onyo Kali kwa kutohudhuria   kikao cha maandalizi ya mechi. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili. Vilevile timu ya Mashujaa imepigwa faini ya sh 200,000 (laki mbili) kwa kupitia mlango usio rasmi wakati wa kuingia uwanjani. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(140 ya Ligi Daraja la Pili.

 

Matukio na uamuzi ligi daraja la kwanza
Hatua ya kwanza ASFC kushika hatamu