Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasha mtambo (pampu) wa kutoa maji chini ya ardhi kwenye kisima kirefu (m 450) kwa ajili ya kuyapeleka kwenda kwenye tanki kubwa la maji eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuwasha mtambo wa kusukuma maji kwenye tanki kubwa la maji kwa ajili ya usambazaji kwa wakazi wa maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuzindua Mradi wa maji Kigamboni ambao unatoa maji lita milioni 70 kwa siku.
Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelekezo mbele ya Rais Samia kuhusiana na mradi mkubwa wa maji ya visima 7 ambao unatoa maji zaidi ya lita milioni 70 kwa siku kwenye hafla iliyofanyika Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso pamoja na viongozi mbalimbali wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi na ugawaji wa magari ya mitambo kwa ajili ya kuchimbia visima virefu na mabwawa.
Rais, Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya Viongozi na Wananchi kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa maji Kigamboni.

NECTA yatakiwa kuimarisha usimamizi changamoto za mitihani

Rais, Samia akiagana na Viongozi pamoja na Wananchi baada ya kuzungumza nao kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa maji Kigamboni Novemba 11, 2022.
Ajali nyingine Lori la mafuta, 12 wafariki
Vikosi vya Jeshi, M23 waanzisha mapigano upya