Kamati ya Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (UNCTAD), imetoa mapendekezo ya sera tatu zinazoweza kutumiwa na nchi zinazoendelea, kufuatia kuongezeka kwa matumizi ya sarafu za kidijitali wakati huu ambapo nchi nyingi hazina sera wala mifumo madhubuti ya udhibiti na matumizi yake kwa jamii.

Kamati hiyo ya UNCTAD imesema, kuibuka kwa janga la Uviko-19 Duniani na watu kujitenga kulisababisha ugumu wa kufanya biashara, manunuzi na utumaji wa fedha kwa familia kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Imesema, “Kutokana na mattizo haya njia mbalimbali zilitumika hali iliyofanya hata nchi ambazo hapo awali zilikuwa hazitumii sarafu za kigijitali ‘Cryptocurrency’ kuanza kuzitumia hivyo ni vyema sasa wakaanza kutumia muongozo huu.”

sarafu za kidijitali

UNCTAD, imetoa miongozo mitatu ya kisera inayomulika hatari ambazo zinaangazia hatua za tisho la sarafu hizo kwenye utulivu wa kifedha, uhamasishaji wa rasilimali ndani ya nchi na usalama wa mifumo ya kifedha.

Mshtuko wa hivi karibuni, wa sarafu hizo za kidijitali kwenye soko unaonyesha kuwa kuna hatari za kibinafsi za kuzishikilia, lakini ikiwa benki kuu itaingilia kati ili kulinda utulivu wa kifedha, huenda shida hiyo inayolikabili soko ikawa ya umma.

Hata hivyo, endapo fedha hizo za kidjitali zitasambaa kama njia iliyoenea ya malipo na kuchukua nafasi ya fedha za ndani ya nchi kwa njia isiyo rasmi (mchakato unaoitwa cryptoization), inaweza kuhatarisha uhuru wa kifedha wa nchi.

Katika nchi zinazoendelea, ambazo zina mahitaji yasiyofikiwa ya fedha za akiba na uimara husababisha hatari na kulifanya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kutoa maoni kwamba sarafu hizo za Kidijitali zinaweza kuleta hatari.

Hassan Dilunga kurudi dimbani Januari 2023
Young Africans yatamba kutetea Ngao ya Jamii