Shirika la kutetea waandishi na vyombo vya habari duniani, Reporters Without Borders limeripoti kuwa waandishi wa habari wapatao 50 wamepoteza maisha wakiwa kwenye kazi zao ndani ya mwaka 2020.

Ripoti hiyo inaonesha kwamba kwa mara nyingine tena Mexico imeshika nafasi ya juu miongoni mwa mataifa yaliyo hatari sana kwa waandishi wa habari, ambapo waandishi nane waliuawa mwaka huu wakati wakichunguza matukio ya uhalifu wa kupanga na ufisadi.

Akizungumza kwa njia ya video na Chombo cha Habari cha Deustche Welle, Mkuu wa Kamati ya Usalama wa Waandishi wa Habari ya Afghanistan, Najib Sharifi, amesema kuwa nchi hiyo haijawahi kuwa ya kutisha kama ilivyo sasa, kwani kwa sasa kila mwandishi wa habari yuko hatarini.

“Ndani ya kipindi cha wiki sita, Afghanistan imeshapoteza waandishi wanne wa habari, na wote waliuawa kwa risasi au kwa mabomu yaliyotegeshwa kwenye gari zao” amesema Sharifi.

Kwa mujibu wa Shirika la Waandishi wa Habari Wasiokuwa na Mipaka, RSF, katika ripoti yake hiyo ya pili kutolewa, hali ni hivyo hivyo kwenye kwenye maeneo mengine duniani.

Ingawa idadi ya waandishi wanaouawa wakiwa wanaripoti matukio ya mapigano imepungua, wale wanaouawa kwa kudhamiriwa imeongezeka maradufu.

Inter Milan kutupa ndoano Hellas Verona
Magufuli awanyooshea kidole TRA