Kiungo kutoka nchini England na klabu ya Tottenham Dele Alli, atakua nje ya uwanja kwa majuma kadhaa, kufuatia jeraha la goti alilolipata akiwa katika mazoezi.

Meneja wa Spurs Mauricio Pochettino, amethibitisha taarifa za kuumia kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, na ilikua sababu ya kutomchezesha katika mchezo wa jana dhidi ya Arsenal ambao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Pochettino alisema mbele ya waandishi wa habari kuwa: “Alli amepatwa na jeraha la goti tulipokua katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Arsenal, aligongana na mwenzake.”

“Niliamini huenda lisingekua tatizo kubwa baada ya kuanguka na kulalama juu ya maumivu yaliyomkabili, lakini kwa ushauri uliotolewa na madaktari, hatokua nasi kwa kipindi cha majuma kadhaa.” Aliongeza Pochettino.

Taarifa za kuumia kwa Alli zimekuwa sababu ya kuachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England, ambacho mwishoni mwa juma hili kitacheza dhidi ya Scotland na siku ya jumanne ya juma lijalo kitapambana na Hispania.

Super Mario Amuita Mamadou Sakho Ufaransa
TB Joshua atabiri mshindi wa Urais wa Marekani na majanga yatakayomkuta