Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Dmitry Muratov ambaye alipiga mnada medali yake ya dhahabu ili kuchangisha fedha kwa ajili ya wakimbizi watoto Juni 20, 2022 amesema kitendo cha medali yake kuvunja rekodi kwa kuuzwa dola milioni 103.5, kimethibitisha kuwa ubinadamu huja pamoja kwa kuonesha mshikamano.

Amesema, yeye na wenzake walipanga kupeleka fedha za tuzo hiyo kwenye mfuko wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), kwakuwa lina ubora wa kazi ya kuhakikisha misaada inawafikia watoto wote wa Ukraine wenye uhitaji.

“Natumaini watoto wa Ukraine ambao sasa walikuwa nchini Urusi, pia watafaidika maana kuna kazi zaidi ya wakimbizi milioni moja na nusu nchini Urusi na tuliichagua UNICEF ambayo ina fursa kama hizo na inaelewa vyema kwamba haina ajenda za kisiasa, bali za kibinadamu,” amesema Muratov.

Mshindi huyu wa Tuzo ya Nobel ambaye ni raia wa Urusi, alitunukiwa nishani ya dhahabu mwezi Oktoba 2021, pamoja na mwanahabari Maria Ressa wa Ufilipino, kutokana na kuhamasisha uhuru wa kujieleza na kuripoti bila woga licha ya unyanyasaji na vitisho vya kuuawa.

Muratov alisema, kulikuwa na maombi toka UNICEF kabla ya mnada huo, na kwamba walifanya uchunguzi wa kina kwa wazabuni mbalimbali, ili kuhakikisha chanzo cha fedha hizo hazijatokana na operesheni yoyote haramu ya uhalifu kama vile binadamu au biashara ya dawa za kulevya.

“Waliangaliwa kupitia mfumo wa benki, mfumo wa kifedha, na yote ambayo ninaweza kusema kwa asilimia 100, ambayo pia niliarifiwa na kuoneshwa kwamba hili ni jambo la uwazi kabisa, na ni fedha halali.

Muratov ni mhariri mkuu wa kampuni huru ya habari ya nchini Urusi, Novaya Gazeta ambayo ilifungiwa na Kremlin mwezi Machi kufuatia vikwazo vipya kwa waandishi wa habari kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Redondo kuondoka Biashara United Mara
Deo Kanda: Nipo tayari kurudi Simba SC