Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde ameandaa tamasha la kudumisha utamaduni liitwalo ‘Mavunde na utamaduni wetu’ lililofanyika mjini Dodoma likiwa na lengo la kuenzi, kulinda na kuhifadhi utamaduni wa watu wa Dodoma.

Aidha, Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, amesema uwepo wa shindano hilo ni utekelezaji wa ahadi yake ambayo aliitoa wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu 2015 na kumpongeza  Rais Dkt. John Magufuli kwa kuhamishia shughuli za serikali Dodoma, kupiga vita Rushwa na Ubadhirifu na Kulinda Maliasili za Taifa kwa manufaa ya watanzania wote.

“Tamaduni zetu zilikuwa zimeanza kusahaulika, watu hawakuona tena umuhimu wa ngoma za jadi na hii ni kutokana na utandawazi na kuwa watu wa mjini sana tumesahau tumetoka wapi,” amesema Mavunde

Vile vile Mavunde amesema katika kampeni hizo aliahidi kwa nafasi yake atajitahidi kuviunganisha vikundi vya kiutamaduni vya kutoka maeneo mbalimbali ili kuenzi na kulinda utamaduni wa Dodoma.

 Hata hivyo, kwa upande wake, Chifu wa Dodoma mjini, Lazaro Chihoma amempongeza mavunde kwa kuandaa tamasha hilo na kudai kuwa wamepita viongozi wengi lakini hawakuona umuhimu wa kuenzi utamaduni wao.

 

Prof. Mbarawa awapa neno wakufunzi wa vyuo
Mke wa Waziri Mwakyembe afariki dunia

Comments

comments