Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imetetea maagizo yanayoruhusu mawaziri kulipwa mishahara na marupurupu kwa maisha yao yote.

Katika taarifa iliyotolewa na serikali ya nchi hiyo, imesema kuwa malipo hayo sio ya kuwatajirisha maafisa na viongozi hao bali ni kuwafanya waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Maagizo hayo, yanayoruhusu mawaziri kupokea marupurupu ya kiwango cha juu zaidi yameshutumiwa vikali, huku idadi kubwa ya raia nchini Congo wakiwa ni maskini.

Aidha, Serikali inayoondoka madarakani ilikuwa inawalipa mawaziri kiwango cha chini kuwatosheleza mahitaji yao ya kimsingi, kama vile chakula, makaazi na huduma ya afya.

Maagizo hayo mawili yaliyotiwa saini na waziri mkuu anayeondoka madarakani, Bruno Tshibala mnamo Novemba, yaliripotiwa pakubwa hivi karibuni katika vyombo vya habari. huku mshauri wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Joseph Kabila amesema kuwa malipo hayo hayaendani na uchumi na jamii nzima.

Rais mpya wa Jamhuri ya Kidmeorasi ya Congo, Felix Tshisekedi, aliapishwa mwezi uliopita, akipokea wadhifa huo kwa amani kutoka kwa Kabila baada ya miaka 60 kupita.

 

 

Taharuki bungeni: Wabunge wakimbia, mwenyekiti asitisha kikao
Wafanyabiashara 10 wakamatwa sakata la watoto kuuawa Njombe