Wakati joto la kusubiri rais John Magufuli atangaze majina ya baraza lake la mawaziri, baadhi ya majina yametajwa kuvuja kutoka kwenye orodha hiyo.

Mmoja kati ya majina ambayo yamevuta usikivu wa wengi ni jina la aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, Bernard Membe alikuwa mmoja kati ya wagombea wa CCM waliokuwa wanatajwa kuwa chaguo la rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa chanzo cha gazeti la Mwana Halisi, majina mengine yanayotajwa ni pamoja na January Makamba na Dk. Asha Rose Migiro.

Jina jipya lililotajwa kwenye orodha hiyo ni jina la aliyekuwa Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT), Dk. Charles Kitima. Dk. Kitima alikuwa mmoja kati ya watu waliomuamini sana Dk. Magufuli wakati akiwa Waziri wa Ujenzi na hata kumualika kuwa mgeni rasmi kwenye mahafari ya chuo hicho.

Hata hivyo, rais Magufuli anatarajiwa kutangaza baraza lake la mawaziri muda wowote kuanzia sasa. Kwa mujibu wa katiba, rais anapaswa kutangaza baraza lake kabla ya kuanza kwa vikao vya bunge vya mwezi Januari.

Picha: Msanii achomwa visu akiwa kazini, mashuhuda wadhani ni Igizo
Mwenyekiti Wa UWT (CCM) Ahamia Chadema