Mawaziri watano na Naibu waziri Mmoja wa Serikali ya awamu ya tano wamenusurika kujiondoa kwenye nafasi zao baada ya kupewa saa chache na Rais John Magufuli kuhakikisha wanawasilisha katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Tamko la Rasilimali, Maslahi Madeni pamoja na Uadilifu .

Agizo hilo la Rais kwa mawaziri hao lilitolewa leo mchana na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Mawaziri hao na Naibu waziri walifanikiwa kuziokoa nafasi zao baada ya kupishana kwenye mlango wa Kamisha wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwasilisha fomu zao mapema wakiiwahi ‘deadline’ iliyotangazwa.

Taarifa iliyotolewa jioni na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu imeeleza kuwa hadi kufikia saa 9 na nusu alasiri, Mawaziri wote pamoja na Naibu waziri huyo walikuwa wameshawasilisha fomu hizo kama walivyoagizwa.

Mawaziri hao ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga,  Waziri wa Nchi ( Muungano na Mazingira), January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, pamoja na Naibu Waziri wa  Nchi (Muungano na Mazingira), Bw. Luhaga Mpina.

1

Hata hivyo, Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga aliirushia lawama Sekretarieti hiyo kwa kupoteza fomu zake kwani alikwisha wasilisha, lakini aliwasilisha fomu nyingine.

Coastal Union Yakiangusha Kigogo Kingine
UEFA Yachezesha Droo Ya 16 Bora Ya Europa League